MAKALA: KWA UBABE HUU WA NJOMBE MJI IPO SIKU.


-Klabu ya Njombe Mji ni mojawapo ya vilabu vitatu vilivyopada ligi kuu msimu uliopita. Katika historia ya ligi kuu Tanzania Bara hii ni mara ya kwanza kwao kushiriki ligi kuu Tanzania Bara kuliko wenzake (Lipuli na Singida) ni vilabu vya zamani ambapo zilishiriki Ligi kuu miaka ya nyuma na zikashuka.

-Ukiangalia msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara mpaka sasa Njombe mji ni wa mwisho kwenye msimamo wa Vodacom Premier League wana pointi 15 baada ya kucheza michezo  19 wameshinda michezo 2 wametoa sare michezo 9 na kufungwa michezo 8.

-Katika michezo 19, Njombe mji wamecheza michezo 10 nyumbani katika uwanja wao wa Sabasaba na 9 wamecheza ugenini. Katika mechi 10 za nyumbani wameshinda mchezo 1, wametoa sare mechi 4 na wamefungwa mechi 5 katika dimba lao la nyumbani la sabasaba tukiambiwa leo ligi kuu iishe Njombe mji wanashuka daraja.

-Nilitaka nikuandikie data na uone uwezo wa Njombe Mji msimu huu namna wanavyofanya kwenye ligi kuu. Njombe Mji naweza kusema msimu huu ndio timu ambayo imeonesha ubabe nje ya uwanja mashabiki wao wanaojiita mabaunsa wameucheza sanà mpira nje ya uwanja kuliko hata wachezaji walivyocheza ndani ya Uwanja. Sijawahi kuona timu mbabe kwenye ligi kuu Tanzania bara kama Njombe Mji.

-Wamekuwa na muendelezo wa matukio ya kibabe yasiyokuwa na tija kwenye soka letu juzi kwenye mchezo dhidi ya Majimaji wao walianza mechi mapema tu huko nje ya uwanja kwa kupambana na mashabiki wa Majimaji pamoja na wachezaji mpaka ikapelekea mchezaji Paul Maona kuumizwa vibaya na kushindwa kucheza mchezo huo.

-Hawa Njombe Mji wanajiamini na wanaamini mambo ya uchawi na ukienda kwenye uwanja wao wanataka wakufanye ujione kama sio Mtanzania wanakutisha wanakupangia mambo yao kama wanavyotaka ila ukikubali tu watakunyanyasa kama wanavyotaka yaani wao wanajifanya  ndio wenye Vodacom Premier League wakiwa pale Sabasaba.

-Njombe Mji wanatoka mkoa wa Njombe wao wana Utajiri wa mabanzi ila sasa ndio wanayatumia kama silaha zao kupambana na wageni wanaoenda katika dimba la Sabasaba sijawahi ona timu ya ovyo ovyo kama Njombe Mji ubabe tu na matokeo ya uwanjani hawapati kwa ubabe huu sitashangaa  nikawaona wanashuka daraja msimu ujao.

-Ni ujinga wa Lami kucheza mechi nje ya uwanja na huko uwanjani hamna kitu wachezaji wao wote wakiwa uwanjani  wanarukaruka tu  kama Mavugo unategemea nini watasalia kweli kwenye ligi kuu hawa? Wanajifanya wao ndio wababe na wanadiriki sasa kuufanya mchezo wa soka uwe vita.

-Daah sijui ile kamati yetu ya Masaa 72 mpaka leo iko kimyaa. Ni ujinga mkubwa kwa viongozi wa Njombe Mji kuunga fujo zinazofanywa na mashabiki wao yaani sijawahi kuona upuuzi kama huu unaofanywa na Njombe Mji hivi Njombe mji wakishuka daraja watakuja kumlaumu mtu kweli? Maana wao sasa ubabe na Mabanzi yao na wanasahau hata kuandaa timu kiushindani. viongozi wa Njombe hata kukemea hamna au wao ndio wanawatuma? ila ukiwahoji kama wanabariki hizi fujo

-Alihojiwa afisa habari wao analalamika shabiki wa Majimaji kutoa taulo kwenye goli ila halaani upuuzi walioufanya wa kuwashambulia mashabiki na wachezaji wa Majimaji sasa ndio tuseme na wao wanabariki huu ujinga kufanyika? Badala ya kutafuta fedha za kuihudumia Timu wao wanahangaika kutafuta mabanzi ya Vita.

-Niliwaona Pia kwenye mechi dhidi ya Simba uwanja wa Uhuru wababe kweli, mechi dhidi ya Yanga pale Sabasaba wanajiona watemi kweli tena mbele ya Yanga, najua waliyowafanyia Azam Fc na Singida United kwa mechi zilizofanyika pale Sabasaba wanapenda sana Fujo hawa watu na huku kwenye mpira sisi sio watu wa Fujoo.

-Timu lao lina shida kubwa hamna fedha wanahangaika kucheza mechi nje ya uwanja? Sijawahi ona mimi timu hata hawana uhakika wa kula milo 3 kwa siku, timu hata mafuta kwa ajili ya kusafiri kwenda kucheza mechi za ugenini hamna, Posho hamna, Mishahara hamna, harafu unahagaika na mambo ya nje ya uwanja.

-Naamini kuna baadhi ya watu pale Njombe ni makini waambieni mashabiki zenu na viongozi zenu wamepanda ligi kuu wapo VPL kwa sasa  hawapo daraja la kwanza (fdl) waambieni hii ni Vodacon Premier League kujifanya kama wako ligi daraja la kwanza (FDL) kutacosti. huku hakufai maana mikamera hadi chooni fujo zao waambieni wazitunze wakishuka daraja ndio wakafanye ubabe huko daraja la kwanza kama walizoea.

-Kwa ubabe huu wa Njombe Mji sitashangaa wakishuka daraja msimu ujao Kila Kheri Njombe Mji.

@yossima Sitta Jr.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.