Ujumbe Wa Kocha Lechantre Kwa Simba Baada Ya Kuondoka

Baada ya kuonekana akiwa uwanja wa ndege Jijini Nairobi Kenya huku akiripotuwa kuikacha klabu ya Simba kocha mkuu wa klabu hiyo, Pierre Lechantre ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram unaoweza kuwa tafsiri kamili ya mustakabli wake ndani ya klabu hiyo.

Katika ujumbe huo wa Lechantre amewaagiza Simba kuhakikisha wanatwaa ubingwa huku akijivunia kile alichokipata akiwa na klabu hiyo.

"Maumivu humfanya mtu kuwa imara, machozi humfanya mtu kuwa imara, kuvunjika moyo humfanya mtu awe na busara au mwenye busara, hivyo shukuru yaliyopita kwa kesho bora au maendleo ya kesho. Si chochote lakini mafanikio mazuri kwa Simba kwenye fainali. Nendeni mkachukue Kombe."

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.