DJUMA: Yaliyopita Si Ndwele, Tugange Yajayo...
Akizungumzia sare ya goli 2-2 dhidi ya Mwadui FC, Djuma amesema: "Tulijaribu kucheza, lakini tulifanya makosa hasa katika kulinda na wapinzani wakaitumia nafasi hiyo kusawazisha. Wachezaji wangu walifanya makosa mengi sana ambayo yalisababisha timu yangu kushindwa kufikia malengo ya kuondoka na pointi 3, lakini wakati mwingine naamini uzembe huu hautajirudia, "alisema,Djuma
Aidha Djuma aliwamwagia sifa vijana wa Mwadui kutokana na mchezo waliouonyesha dhidi ya Simba "Nadhani Mwadui walicheza vizuri sana na unapaswa kutoa pongezi kwao. Katika soka na katika michezo, chochote kinaweza kutokea. Bila shaka, tunaweza kupoteza leo lakini usikate tamaa, kwa sababu haujui nini kitatokea baadaye. "Aliongeza Djuma
Simba kwa sasa ipo nchini Djbout ambako imekwenda kucheza mchezo wa marudiano na klabu a Gendarmeria ya nchini humo katika michuano y kombe la Shirikisho barani Afrika.