TAMKO LA YANGA KUHUSU YOUTHE ROSTAND KUSHIRIKI MICHUANO YA KOMBE LA KLABU BINGWA...



Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa tamko kuhusu tetesi za jina la mlinda mlango Youthe Rostand kuwa halikutumwa kwenye usajili wa CAF.

Kupitia kwa Meneja wa klabu huyo, Hafidh amesema kuwa hakuna ukweli wowote kwenye taarifa hizo,jina la golikipa huyo lilitumwa na leseni yake kwa ajili ya kucheza mashindano ya klabu bingwa tunayo.


Ni uzushi tu usiokuwa na maana,jina la Rostand lilitumwa CAF na leseni yake ya kucheza mashindano tunayo, hivyo siyo kweli kwamba jina lake halikutumwa,kuhusu kucheza au kutokucheza mchezo,siku zote benchi la ufundi ndiyo hupanga kulingana na mipango ya mchezo husika.

Yanga wataondoka hapa jumapi ili kuekea huko Shelisheli. 

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.