MZUNGUKO WA NNE WA KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM KUANZA LEO
Hatua ya mzunguko wa Nne(4) wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam inatarajia kuanza leo Jumatano Februari 21, 2018.
Kwenye Uwanja wa Sabasaba Njombe kutakuwa na mchezo mmoja utakaowakutanisha mwenyeji Njombe Mji atakayecheza dhidi ya Mbao FC kutoka Mwanza saa 10 jioni.
Mechi nyingine za Kombe la Shirikisho la Azam zitaendelea Jumamosi Februari 24,wakati Singida United watakapowakaribisha Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Namfua saa 10 jioni na KMC watawaalika Azam FC saa 1 usiku Azam Complex.
Jumapili Februari 25, 2018 Buseresere watakuwa uwanja wa Nyamagana Mwanza saa 8 mchana kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro,Majimaji FC ya Ruvuma watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Majimaji kuwakaribisha Young Africans ya Dar es Salaam saa 10 jioni wakati Ndanda FC watakuwa ugenini kucheza na JKT Tanzania saa 1 usiku Azam Complex Chamazi.
Jumatatu Februari 26, 2018 kutachezwa mechi mbili Kiluvya United dhidi ya Tanzania Prisons saa 8 mchana Uwanja wa Mabatini na Stand United watawaalika Dodoma FC saa 10 jioni uwanja wa Kambarage.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.