HARUNA NIYONZIMA AWASILI INDIA KWA AJILI YA MATIBABU
Baada ya Mchezaji wa Klabu ya Simba Haruna Niyonzima kukaa nje ya Uwanja kwa Juma kadhaa kutokana na kuwa Majeruhi sasa ameenda Nchini India kwa ajili ya Matibabu ya Mguu wake wa kulia unaomsumbua.
Haruna aliondoka jana hapa Nchini na kuelekea India na Leo Asubuhi amefika Nchini humo kwaajili ya Mtibabu yake.
Akizungumza na Wordsports14 kwa njia ya Simu Haruna amesema kuwa anamshukru Mungu amefika Salama India alikoenda kutibiwa na kuwasihi wapenzi na Mashabiki wake wamuombee apone haraka ili arudi Uwanjani kuwapa Burudani walioikosa kwa mda kadhaa kutoka kwake. "Niliondoka Jana Tanzania na leo Asubuhi nimefika salama India kwa ajili ya matibabu yangu ya Mguu,Kikubwa niwaombe wapenzi na Mashabiki wa Simba SC waniombee nipone haraka ili nirudi Kuwafanyia kazi nzuri"amesema Haruna
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.