Watano Simba waitwa timu za taifa, Yanga wao watazamaji tu.
Wakati maproo watano wa Simba wakiitwaa katika timu zao taifa wenzao wa Yanga watakuwa watazamaji wiki ijayo katika michezo ya kusaka kufuzu kwa fainali Mataifa ya Afrika 2019, Cameroon.
Habari njema kwa Simba ni pamoja na wachezaji wake Cloutous Chama, Haruna Niyonzima pamoja na beki Murushid Juuko kutoichezea klabu hiyo bado makocha wa timu za mataifa yao kujiandaa na mechi kusaka kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwakani.
Kocha wa Rwanda, Vincent Mashami amemwita mshambuliaji Meddie Kagere na kiungo Niyonzima katika kikosi chake kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Ivory Coast utakaochezwa Septemba 8.
Naye kocha wa Uganda Cranes, Sebastien Desabre amewajumuisha kikosini mshambuliaji Emmanuel Okwi na beki Murushid Juuko wote wa Simba kujiandaa na mchezo dhidi ya Tanzania.
Kiungo mpya wa Simba, Mzambia Chama akiwa bado hajapata nafasi ya kucheza katika mechi za mashindano nchini, lakini kocha wa Chipolopolom Van Vandenbroeck amemwita katika kikosi chake cha wachezaji 26 kitakachocheza dhidi ya Namibia wiki ijayo jijini Windhoek.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.