Yanga kuelekea Rwanda siku hii
Wawakilishi pekee kutoka Tanzania katika mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika (Caf Confederation Cup) klabu ya Yanga itaondoka siku ya Jumatatu August 27 kuelekea Rwanda kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda mchezo utakaochezwa siku ya Jumatano August 29.
Baada ya Mchezo huo kuchezwa klabu ya Yanga itaelekea Shinyanga moja kwa moja kwaajili ya mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui Fc mchezo utakaochezwa Jumapili ya September 02 katika dimba la CCM kambarange Mkoani Shinyanga.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.