Yanga Kuisaka Nafasi Ya Pili Leo..
Klabu ya Yanga leo inatarajiwa kushuka dimbani kutupa karata yake nyingine fhifi ya Mbao fc katika mchexo wa ligi kuu Tanzania bara ili kuona kama inaweza kujisogeza mbele na kutwaa walau hata nafasi ya pili.
Yanga ambayo imekuwa na mwenendo mbaya tangu alipoondoka aliyekuwa kocha wake mkuu, George Lwandamina itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kitopata Ushindi katika mchezo wowote kwenye michezo 9 iliyopita.
Tangazo |
Yanga inatarajiwa kupata Ushindi katika mchezo huo ili kujiwekea mazingira mazuri ya kuisogelea Azam huku ikiiombea ipoteze mchezo wake kabla ya timu hizo kukutana.
Hata hivyo mbao nao watashuka katika mchezo huo wakiwa na imani ya kupata ushindi kutokana na matokeo waliyoyapata mchezo uliopita kwa kuwanyula Stand United ukilinganisha na wapinzani wao Yanga waliopoteza dhidi ya Mwadui.
Aidha Yanga itamkosa beki wake kisiki Kelvin Yondani ambaye anatumikia kifungo baada ya kumtemea mate Asante Kwasi.
Donald Ngoma naye pia ni miongoni mwa wachezaji watakao kosekana kutoka na na majeraha, Amisi Tambwe Na Thabani Kamusoko wao wanatarajiwa kushika nafas.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.