Ushauri Wa Bocco Kwa TFF Na Bodi Ya Ligi.
Bocco wa tatu kutoka kushoto, Nyuma ya Okwi. |
Bocco ameiambia amesema kuwa changamoto kubwa msimu huu ilikuwa ni viwanja vya mikoani kutokuwa na katika ubora mzuri hali iliyofanya mechi kuwa ngumu zaidi.
Nyota huyo wa zamani wa Azam FC ameongeza kuwa asilimia kubwa ya viwanja vya mikoani havina ubora wa kuchezea ligi kitu ambacho kimemsukuma kuishauri TFF kuliangalia suala hilo kwa makini.
"Nadhani TFF na Bodi ya ligi inapaswa kuangalia ubora wa viwanja msimu ujao ili ushindani uwe mkubwa.
"Unajua sisi tunatumia uwanja wa Taifa au Uhuru kwa mechi zetu za nyumbani ubora wake ni mkubwa ndio maana tunapata matokeo ukilinganisha na mikoani," alisema Bocco.
Mshambuliaji huyo anategemewa kuwa miongoni mwa wachezaji wa Simba watakaocheza mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Majimaji siku ya Jumatatu.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.