Azam Yamsainisha Ngoma Mkataba Kimyakimya
Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Azam FC wamemalizana na aliyekuwa Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma kwa kusaini naye mkataba wa mwaka mmoja.
Yanga walishindwa kumvumilia Mzibambwe huyo kwa kusitisha mkataba wake kutokana na kuwa na majeraha ya muda mrefu hali ambayo ilipelekea kushindwa kukitumikia kikosi cha Wanajangwani.
Azam sasa watagharamika kwa ajili ya matibabu ya mchezaji huyo aliyekosekana dimbani kwa takribani msimu mzima wa 2017/18 wakati akiwa Yanga.
Imeelezwa kuwa uongozi wa Azam FC umekuwa ukikanusha kuhusiana na kumsajili mchezaji huyo kimyakimya, lakini taarifa za chini ya kapeti zinaeleza wamemalizana naye.
Ngoma alijiunga na Yanga mwaka 2015 akitokea FC Platnum ya nchini kwao Zimbambwe aliyoanza kuichezea mwaka 2012.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.