Usajili Simba Siri Nzito
Mabingwa wa ligi kuu bara timu ya Simba imekataa kuweka wazi aina ya wachezaji ambao itawasajili kwa ajili ya msimu ujao ambao wataiwakilisha nchi katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.
Simba inajiandaa kufanya usajili mkubwa msimu ujao kwakua imepanga kuhakikisha inafanya vizuri kwenye michuano ili kutimiza kazi waliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli.
Mei 19, Rais Magufuli aliwataka Simba kuhakikisha wanatwaa kombe la ubingwa Afrika ingawa aliwaambia wanahitaji kuimarisha kikosi chao ili kufanikisha jambo hilo wakati akiwakabidhi taji la ubingwa.
Kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesema watafanya usajili mkubwa kutokana na kushiriki michuano mikubwa Afrika lakini amekataa kutaja idara ambazo watazifanyia marekebisho.
"Kuhusu usajili siwezi kulizungumzia kwa sasa, tutasajili kwakua kuna michuano mikubwa mbele yetu lakini muda bado haujafika wakuweza wazi jambo hilo," alisema Masoud.
Wekundu hao wanatarajiwa kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup ambayo itaanza Juni 3 nchini Kenya.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.