TFF HIVI BADO YONDANI AMEFUNGIWA?

Yondani wakwanza kushoto, Asante Kwasi katikati na Andrew Vicent kulia.


-Shirikisho la mpira wa mguu Tanzania (TFF) kupitia kamati ya masaa 72 ilimsimamisha kucheza mechi za ligi kuu beki wa klabu ya Yanga, Kelvin Yondani may 03 kwa kitendo cha kumtemea mate beki wa klabu ya Simba kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara April 29.

-Kelvin Yondani alisimamishwa na kamati ya masaa 72 na suala lake kupelekwa kamati ya Nidhamu na maadili. Yondani hakutokea kwenye kamati ya nidhamu na Kamati hiyo haikutoa hukumu ya shitaka hilo.

-Kwanza siungi mkono kitendo alichofanya Yondani kwa Kwasi. Tangu asimamishwe Yondani amekosa mechi nne za ligi kuu dhidi ya Tz Prisons, Mtibwa Sugar, Mwadui Fc na Mbao Fc na mechi ya leo dhidi ya Ruvu Shooting ni mechi ya tano.

-TFF adhabu ya Yondani ikoje? itakuwaje kama Yondani atakutwa na hatia ya kufungiwa mechi 3 na tayari amekosa mechi 5 Itakuwaje? TFF hawaonei kama hawamtendei haki Kelvin Yondani na mwajiri wake klabu ya Yanga Sc.

-Yanga wamekosa huduma ya Yondani kwa mechi tano bila hata TFF kutoa hukumu. Sheria hizi zipo Tanzania tu za kumsimamisha mchezaji bila kutoa adhabu.

-Hii si mara ya kwanza kwa TFF kumsimamisha mchezaji bila kutoa adhabu yake walishafanya hivyo kwa Abdi Banda msimu uliopita, Obrey Chirwa, Razak Abarola na wengine msimu huu ni sheria za ajabu kuwahi kutokea kwenye soka letu. Huwezi kuta au kuona ligi kuu ya Afrika Kusini mchezaji anasimamishwa bila kutolewa kwa adhabu yake.

-Ni aibu kwa soka letu ni aibu kwa shirikisho la soka letu huwezo ukaendekeza kanuni na sheria za uzwazwa kama hizi. TFF mukimaliza mambo yenu kumbukeni Yondani bado amesimamisha kucheza ligi kuu Tanzania Bara (vpl) na kamati yenu.

@yossima Sitta Jr.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.