MO AMTUMIA STRAIKA TIKETI YA NDEGE
Apaa fasta na kutua Dar Moh'd Rashid naye huyoo Msimbazi
STRAIKA wa Majimaji, Marcel Boniventure, amepanda ndege fasta kutoka mjini Songea na kutua Dar es Salaam jana jioni kumalizana na Simba, baada ya kutumiwa tiketi ya ndege na mfanyabiashara maarufu nchini na mwanachama wa Wekundu wa Msimbazi hao, Mohammed Dewji ‘Mo’.
Boniventure ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakiliumiza vichwa benchi la ufundi la Simba kwa muda mrefu kama ilivyokuwa kwa timu nyinginezo, hasa Yanga, Singida United na hata Azam FC, zilizokuwa zikimpigia hesabu kumtwaa kutokana na kuvutiwa na kiwango chake.

Pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara kutarajiwa kumalizika Jumatatu ijayo, Mo hakutaka kuremba, baada ya kubaini kiu ya timu yake tangu kipindi cha usajili wa dirisha dogo ya kuwa na straika huyo, hivyo juzi alimtumia tiketi ili aweze kutua Dar es Salaam na kumalizana na Wekundu wa Msimbazi hao.
Taarifa ambazo BINGWA lilizipata jana kutoka ndani ya Simba, zilieleza kuwa, klabu hiyo ilipanga kumalizana na Boniventure mjini Songea mara baada ya mchezo wao dhidi ya Majimaji wa kufunga dimba la Ligi Kuu Bara Jumatatu.

Uamuzi huo ulitokana na matakwa ya mchezaji mwenyewe ambaye hakutaka dili hilo lifanyike kabla ya mchezo huo, kuhofia kutajwa kuihujumu timu yake iwapo itapoteza.
Wakati pande hizo mbili zikiwa zimeshakubaliana kumalizana mjini Songea, MO aliamua kukata mzizi wa fitina na kumpigia simu Boniventure kumtaka atue Dar es Salaam kukamilisha suala la mkataba wa awali, kutokana na kuwapo kwa taarifa kuwa Singida United nao walikuwa wakimwinda.

“Mazungumzo ya awali yalishafanyika na alitakiwa kuja Dar es Salaam tangu Jumanne ya wiki hii, lakini mchezaji huyo alikataa kwa kuhofia huenda kutupiwa lawama za kuihujumu timu yake pale ikitokea Majimaji imefungwa na Simba.
“Taarifa hizi zilipomfikia MO, akaamua kumpigia mwenyewe simu na kuongea naye, huku akisisitiza kabla ya mechi ya Simba na Majimaji, suala hili liwe limekwisha.
“Toka usajili wa dirisha dogo, zoezi la kuongea na Marcel lilikuwa likifanywa na Muslay (Muslay Al Ruwah, ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji), baada ya aliyewahi kuwa kocha wetu, Joseph Omog, kumhitaji,” alisema mtoa habari huyo.
Mtoa habari huyo wa uhakika alisema kuwa, hata Mfaransa Pierre Lechantre alipomuona Boniventure katika mchezo wa Simba dhidi ya Majimaji wa mzunguko wa kwanza kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, alivutiwa na kiwango chake na kuutaka uongozi kuanza mazungumzo naye.
Ilielezwa kuwa, Pierre alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa, iwapo straika huyo hatosajiliwa na Simba, yupo tayari kumtafutia timu kwao Ufaransa.
Ilielezwa kuwa, Pierre alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa, iwapo straika huyo hatosajiliwa na Simba, yupo tayari kumtafutia timu kwao Ufaransa.
Kutokana na taarifa hizo, BINGWA lilimtafuta Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, ambaye ndiye anayetajwa kukabidhiwa timu kutokana na Pierre kutokuwa na uhakika wa kuendelea kuinoa timu hiyo msimu ujao, ambaye alikiri Mercel kuwa na uwezo wa kuisaidia Simba kuvuna mabao.
“Ni mchezaji mzuri, kwani kuweza kuifungia timu yake mabao 13 si kitu kidogo, nina uhakika kama atakuja Simba na kupata nafasi, atafanya makubwa zaidi,” alisema Djuma.
“Ni mchezaji mzuri, kwani kuweza kuifungia timu yake mabao 13 si kitu kidogo, nina uhakika kama atakuja Simba na kupata nafasi, atafanya makubwa zaidi,” alisema Djuma.
BINGWA lilimtafuta Boniveture jana, ambaye alikiri kutumiwa tiketi ya ndege juzi na alitarajiwa kuwasili Dar es Salaam jana saa 10:00 jioni.
“Ni kweli hapa tunapozungumza (jana) nipo uwanja wa ndege nataka nipande ndege kuja Dar es Salaam, nina mazungumzo na viongozi wa Simba, wameniita haraka,” alisema.
Alisema kuwa, uongozi wa Majimaji umempa baraka zote za kujiunga na Simba, kwasababu mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
Katika mbio za ufungaji bora Ligi Kuu Bara hadi sasa, Boniventure ni miongoni mwa walioonyesha ushindani mkubwa, baada ya kufunga mabao 13 akiwa nyuma ya John Bocco wa Simba (14), huku Emmanuel Okwi akiongoza kwa kucheka na nyavu mara 20 katika michezo 29 ya ligi hiyo.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.