Nadhani Masau Bwire Amezisahau Goli 7 Awaomba Simba Mechi Ya Kwanza Msimu Ujao



AFISA Habari na Mawasiliano wa maafande wa Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani, Masau Bwire ameiomba bodi ya ligi iwapangie kuanza na mabingwa Simba SC kwenye ratiba ya Ligi Kuu msimu ujao.

Akizungumza kupitia kipindi cha Kumekucha Michezo kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV Bwire alisema wanatamani waanze ‘kuwapapasa’ mabingwa hao ili wadhihirishe mapema ubora wa kikosi chao.


“Tutaiomba Bodi ya Ligi msimu ujao watupangie kuanza mpapaso na Wekundu wa Msimbazi ambao ndio mabingwa wa Tanzania kwani kikosi chetu ni bora kuliko kikosi chochote kwenye ligi kuu,” alisema.

Bwire anayefahamika kwa maneno mengi aliendeleza tambo zake kwa kuwatahadharisha Yanga kuwa wajiandae vizuri kwani Ijumaa wataenda kuwapapasa.


“Yanga wakae tayari kwani tutawapapasa Ijumaa hii, hakuna raha kama kumpapasa mtu mzima,” alimalizia Bwire.

Ruvu na Yanga zinatarajia kuminyana Ijumaa hii ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo Yanga waliobakiwa na mechi mbili mkononi ndio wenyeji wa mtanange huo.

Source:Boiplus

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.