HAWA HAPA WACHEZAJI 30 WANAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA LIGI KUU TANZANIA (VPL) WA MSIMU 2017/2018

Tokeo la picha la OKWI BOCCO SIMBA YANGA


30 Wanaowania Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Ligi Kuu Vodacom 2017/18


TUZO ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kufanyika Juni 23 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar huku tayari majina 30 ya nyota wanaowania tuzo huyo yakiwekwa hadharani.

Akizungumza na wanabari leo Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema Kamati ya Tuzo ya VPL imekamilisha orodha ya wachezaji 30 watakowania tuzo hiyo na kwamba mchakato wa kumpata mshindi unaanza rasmi.

Nyota waliopo katika orodha hiyo ni Habibu Kiyombo, Hamis Mcha, Yahya Zaid, Kelvin Yondani, Razack Abarola, Aggrey Morris, Himid Mao, Awesu Awesu, Adam Salamba, Mohamed Rashid, Shafiki Batambuze, Mudathir Yahya, Marcel Kaheza na Adam Salamba.

Wengine ni Eliud Ambokile, Shabani Nditi, Tafadzwa Kutinyu, Ibrahim Ajibu, Gadiel Michael, Papy Tshishimbi, Obrey Chirwa, Aishi Manula, Emanuel Okwi, John Bocco, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Shiza Kichuya, Asante Kwasi, Hassan Dilunga na Bruce Kangwa.

Vilevile Ndimbo amesema wameamua kufuta tuzo ya Mchezaji Bora wa kigeni ili kuwapa fursa wachezaji wote kuwani tuzo ya mchezaji bora wa jumla badala ya kuwatenganisha.


“Tumeondoa tuzo ya Mchezaji Bora wa kigeni ili tuwape fursa wachezaji wote kuwania tuzo ya mchezaji bora wa VPL. Pia tumeongeza tuzo ya Mwamuzi Msaidizi ambayo haikuwepo msimu uliopita,” alisema.

Wachezaji hao 30 watafanyiwa mchujo ambapo watabakia 10 kisha kufanyiwa tena mchujo na kubaki watatu ambao wataingia kwenye fainali siku hiyo ya mwisho.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.