20 Yanga Kuwafuata Dicha Leo Chini Ya Kocha Mwandila
Jumla ya Wachezaji 20 na Viongozi 13 Kati yao 8 kutoka katika Benchi la Ufundi Wa Klabu ya Yanga SC Wanatarajiwa kusafiri mapema leo kuelekea Nchini Ethiopia Kucheza Mchezo wa Marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wapinzani Wao Wellaita Dicha.
Yanga inakwenda Ethiopia ikiwa tayari na mtaji wa mabao 2-0 iliyopata kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa April 07 kwenye uwanja wa Taifa.
Inahitaji ushindi, sare au kufungwa kwa tofauti isiyozidi mabao mawili ili iweze kufuzu.
Kama itapata goli la ugenini itakuwa imejiweka kwenye nafansi nzuri zaidi ya kutinga hatua ya makundi kwani itailazimu Dicha kushinda zaidi ya mabao matatu.
Katika mchezo huo Yanga itakuwa na wachezaji wake wanne, Kelvin Yondani, Said Juma Makapu, Obrey Chirwa na Papi Tshishimbi waliokosa mchezo uliopita wakitumikia adhabu ya kadi mbili za njano.
Makocha Noel Mwandila na Shedrack Nsajigwa nao watarejea katika benchi baada ya kukaa jukwaani mchezo uliopita kutokana na mkanganyiko uliosababishwa na CAF.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.