Usajili Ulio Kamilika Singida United Msimu Huu.

singida united
Singida United Logo

Klabu ya Singida United ambao wamemaliza katika nafasi ya tatu katika michuano ya Sportpesa iliyomalizika jumapili iliyopita june 10. Tayari Singida imekamilisha usajili wa wachezaji Tibar George kutoka Ndanda Fc, Habib Kiyombo kutoka Mbao Fc, Diaby Amara kutoka Asec ya Ivory Coast, Feisali Salum kutoka JKU ingawa bado hawajamtambulisha rasmi.

Pia klabu hiyo imemrejesha kundini beki wao wa kimataifa wa Zimbabwe, Elisha Muroiwa ambaye aliondoka Singida mwezi December mwaka jana kwa Sababu ya matatizo ya kifamilia pia Danny Lyanga atakuwa huru kuitumikia klabu ya Singida msimu ujao baada ya adhabu yake ya miezi sita kuisha huku Mbrazili Felipe Santos bado hajasaini mkataba.


Baada ya usajili huo klabu ya Singida United itaachana na wachezaji wafuatao kwa sababu mbalimbali Tafadzwa Kutinyu ameondoka klabuni hapo na kujiunga na klabu ya Azam Fc. Mudathir Yahya mkataba wake umeisha na klabu ya Singida United kwa sasa ni mchezaji huru.

Danny Usengimana na Michael Rusheshagonga wote raia wa Rwanda wataachana na klabu hiyo kutokana sababu inayotajwa klabu ya Singida United kushindwa kutimiza matakwa ya kimkataba Danny Usengimana alisajiliwa kwa dau la milioni 200 ila amelipwa milioni 80 tu na zingine hajalipwa mpaka sasa hivyo hivyo kwa Rusheshagonga.

Papy Kambale yeye anaachwa kwa sababu ya kufanya utovu wa nidhamu kila mara ndani ya klabu hiyo. Shafik Batambuze anaachana na Singida United kwa sababu kutotimiziwa matakwa ya kimkataba huku Deus Kaseke akitarajiwa kwenda kufanya majaribio Afrika Kusini ila akifeli anaweza akajiunga na Azam moja kwa moja.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.