AZAM YAIOMBA TFF KUSOGEZA MBELE MECHI YAO YA NJOMBE MJI


Uongozi wa klabu ya Azam FC umeandikia barua Bodi ya ligi (TPLB) kusogeza mbele mechi yao ya kesho dhidi ya Njombe Mji kwakua hawajapata muda wa kupumzika.

Azam imecheza jana na Maafande wa Ruvu Shooting na kukubali kipigo cha mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani.

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd ameiambia SDF Sports kuwa kwa mujibu wa kanuni za ligi timu inatakiwa kupumzika siku tatu (saa 72) kabla ya mechi lakini kama watacheza kesho itakuwa ni saa 48.

"Tumeandika barua kwa Bodi ya ligi kuomba mechi yetu ya kesho isogezwe mbele kwakua hatukupata muda wa pumzika na kanuni hata za FIFA zinasema lazima timu ipumzike siku tatu baada ya mechi," alisema Jaffer.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa kesho saa 1 jioni katika uwanja wa wa Azam Complex uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.