Watatu Yanga Kuwakosa Waethiopia Akiwemo Ajibu.
Kiungo mshambuliji wa timu ya Yanga Ibrahimu Ajibu hakusafiri na kikosi cha Yanga kilichokwenda Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaita Dicha kutokana na kuwa majeruhi.
Yanga imeondoka alfajiri ya leo kuelekea Ethiopia tayari kwa mchezo utakaofanyika Aprili 18.
Mbali na Ajibu nyota wengine watakaokosa mchezo ni mlinda mlango Ramadhan Kabwili na Said Mussa ambao wapo kwenye kikosi cha timu ya vijana ya Ngorongoro Heroes.
Kikosi cha Yanga kilichosafiri makipa ni Youthe Rostand na Benno Kakolanya.
Walinzi ni Hassan Kessy, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Gadiel Michael, Abdalah Shaibu, Kelvin Yondani na Nadir Haroub.
Viungo ni Raphael Daudi, Papy Tshishimbi, Pius Buswita, Said Juma, Thaban kamusoko, Yusuph Mhilu, Geofrey Mwashiuya na Emmanuel Martin
Washambuliaji ni Obrey Chirwa, Juma Mahadhi na Yohana Mkomola.
Yanga itaingia katika mchezo huo ikiwa na faida ya mabao 2-0 kufuatia ushindi iliyopata kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika uwanja wa Taifa Aprili 7.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.