Singida Wakanusha Usajili Wa Ndayiragije
Siku tatu zilizopita klabu hiyo ilitangaza kuwa haitendelea na Hans baada ya kufikia makubaliano na kukazagaa taarifa kuwa Ettiene ndiye mrithi wake kwenye timu hiyo ambayo imepanda daraja msimu huu.
Mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyo, Festo Sanga amesema makocha wengi wengi wametuma maombi kuitaka nafasi hiyo na Uongozi unapitia kabla ya kutoa maamuzi ya mwisho.
"Bado hatujamalizana na kocha yoyote, tumepokea maombi kutoka kwa makocha wengi kutaka kufanya kazi nasi, Uongozi unapitia CV zao.
"Tutaweka wazi kila kitu muda ukifika, kwa sasa tunajiandaa na mchezo wetu wa fainali ya FA dhidi ya Mtibwa Sugar mwezi ujao," alisema Sanga
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.