MZEE KILOMONI ATOA KAULI TATA MBELE YA MANARA

Image may contain: 1 person, smiling, outdoor



-Aliyekuwa mjumbe wa baraza la wadhamini la klabu ya Simba, Mzee Hamisi Kilomoni ametoa kauli tata mbele ya Mkuu wa kitengo Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara kuelekea mechi ya kesho ambayo klabu ya Simba itakabidhiwa kombe na Rais Dk John Pombe Magufuli.

-Mzee Kilomoni ambaye leo alikuwepo kwenye mkutano wa waandishi wa habari na mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda na Haji Manara alianza kushukuru ujio wa Rais Dk Magufuli kuhudhulia mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Kagera baada ya mchezo huo kutakuwa na halfa ya kukabidhiwa kombe klabu ya Simba na Rais Dk Magufuli.


-Baada ya kushukuru Mzee Kilomoni alisema yeye ni Mjumbe wa baraza la wadhamini wa klabu ya Simba mpaka sasa na hatambui kama aliondolewa kwenye Baraza hilo. Baada ya kusema hivyo Mzee Kilomoni akawaasa wanachama wa klabu ya Simba Sc yeyote ambaye atajitokeza na kuleta ubaguzi ndani ya klabu hiyo basi atakuwa hayuko pamoja na klabu hiyo.

-Mzee Hamis Kilomoni alitolewa kuwa mjumbe wa baraza la wadhamini wa klabu hiyo August 2017 na nafasi yake kuteuliwa Adam Mgoyi kwa kosa la kufungua kesi mahakamani kwa ajili ya kuzuia mkutano wa mabadiliko ya katiba ya klabu hiyo kuhusu mfumo wa uendeshaji wa klabu.

-Hii ni kauli tata kuelekea mkutano wa mabadiliko keshokutwa jumapili ya May 20 katika ukumbi wa Mikutano wa JK Nyerere uliopo Ocean Road Posta Dar. Na hivi karibuni Msemaji wa klabu ya Simba aliviasaa vyombo vya habari kuacha kuwahoji na kuwasapoti watu wanaopinga mfumo wa uwekezaji ndani ya vilabu vya Simba na Yanga.

-Haijajulikana Mzee Kilomoni alikuwa anamlenga nani kwa kauli yake maana alienda mbali na kusema kwa sasa wamefanikiwa kuchukua Ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara kutokana na umoja waliokuwa nao klabu ya Simba na hawatakubali mtu alete ubaguzi ndani ya Klabu hiyo.

@yossima Sitta Jr.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.