Baada Ya Kugonga Mwamba Kwa Salamba, Yanga Yageuzia Majeshi Kwa Nyota Hawa..
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa tayari imeshamalizana na wachezaji watatu watakao ongezwa kwenye kikosi cha Yanga kwa ajili ya michuano ya Kimataifa.
Mkwasa ametoa kauli hiyo leo ikiwa ni siku moja imepita tangu klabu ya Lipuli FC igome kumtoa mshambuliaji wake Adam Salamba.
Mkwasa amesema wataweka majina ya wachezaji hao hadharani wakati muafaka ukifika baada ya kubaini kuna timu zimedhamiria kuvuruga mipango ya usajili ya klabu hiyo.
Yanga inaruhusiwa kuongeza hadi wachezaji watatu katika kikosi chake kinachoshiriki hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Kwa habari zaidi Download App ya Mwana Jangwani kutoka Play Store. Bonyeza picha hapa chini
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.