Kocha Mkuu Yanga Arejea Kwao Congo, Mkwasa Asema Haya..

Tokeo la picha la kocha mpya yanga 2018 sokakiganjani


Katibu wa klabu ya Yanga, Boniface Mkwasa amethibitisha kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Mwinyi Zahera ameondoka klabuni hapo na kurudi kwao DRC Congo kuifundisha timu ya taifa ya DRC Congo.

-Kabla ya kujiunga na klabu ya Yanga kocha Mwinyi Zahera alikuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya DRC Congo na alikuja kuchukua nafasi ya kocha George Lwandamina aliyeondoka kwenda kwao Zambia kuifundisha timu ya Zesco United ya Zambia


-Zahera ambaye amekuwa akiifudisha klabu hiyo tangu mchezo wa Simba Sc inadaiwa bado hajasaini mkataba na klabu hiyo ingawa makubaliano ya kimkataba yalishakubaliwa makubaliano yalikuwa asaini mkataba wa miaka miwili atakaokuwa analipwa milioni 12 kwa mwezi.

-Zahera ameenda kwao Congo kwa ajili ya kukiandaa kikosi cha taifa ya DRC Congo ambacho kina mchezo wa kirafiki na Timu ya DRC Congo. Habari kutoka ndani ya Yanga viongozi wa Yanga wamegawanyika kuhusu kumpa mkataba kocha huyo.

@yossima Sitta Jr.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.