Mtibwa Haooo Kimataifa Dilunga Awaahidi Haya..



Kiungo mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Hassan Dilunga amewaahidi wapenzi na mashabiki wa Wakata miwa hao ubingwa wa kombe la FA katika mchezo wa fainali utakao fanyika Juni 2 jijini Arusha.

Mtibwa itakutana na Singida United katika fainali hiyo itakayofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Dilunga ambaye jana alifunga bao pekee katika mchezo dhidi ya Njombe Mji amewataka mashabiki wa Mtibwa kujitokeza kwa wingi jijini Arusha kuipa hamasa timu ili kuibuka na ubingwa.

"Sisi wachezaji tumejipanga kuhakikisha tunashinda mchezo wa fainali dhidi ya Singida kikubwa tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi.

"Nadhani ni zamu yetu kuibuka mabingwa wapya wa FA, uwezo tunao na tumejipanga kufanya hivyo," alisema Dilunga.

Nyota huyo wa zamani wa timu za Yanga na Ruvu Shooting yupo kwenye kiwango bora na amekuwa msaada mkubwa kwa vijana wa kocha Zuberi Katwila msimu huu.

Ikumbukwe pia endapo mtibwa watatwaa  ubingea huo basi ndio watakaokuwa wawakirishi wa nchi Kimataifa

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.