MO KUAMUA HATIMA YA LECHANTRE SIMBA

Image may contain: 1 person, standing, outdoor and nature

Jana wanachama wa klabu ya Simba wameridhia kwa pamoja kubadili katiba ya klabu hiyo na kuingia kwenye mfumo wa hisa ambao wanachama wa klabu hiyo watamiliki asilimia 51 huku mwekezaji aliyeshinda tenda Mohamed Dewji 'Mo' kumiliki asilimia 49.

-Kuanzia msimu ujao Simba itakuwa inaendeshwa kwa utaratibu mwingine kabsa wa mfumo wa hisa. Wakati timu ikiingia kwenye mfumo wa hisa hatima ya kocha mkuu wa klabu Pierre Lechantre iko mikononi mwa mwekezaji wa klabu hiyo Mohamed Dewji.


-Pierre Lechatre raia wa Ufaransa alisaini mkataba Simba January 19 ikiwa ni mkataba wa miezi 6 anaolipwa milioni 30 kwa mwezi ambao utaisha July 30. Kuanzia August 01 Mwekezaji Mohamed Dewji ndio ataamua kumuongeza mkataba Lechantre au kumruhusu aondoke.

-Kocha Pierre Lechatre ameomba kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Cameroon iwapo atapata kazi hiyo klabu ya Simba itaachana naye moja kwa moja lakini asipopata kazi klabu ya Simba kupitia kwa Mo itaamua Hatima yake kuondoka, Kuongezewa mkataba au kubadilishiwa majukumu.

-Mjumbe wa kamati tendaji wa klabu hiyo ambaye ni rafiki wa karibu wa Mohamed Dewji amesema Mwekezaji Mo amepanga kuajiri makocha wenye sifa kwa timu zote za Simba timu ya wakubwa, timu ya vijana na timu ya wanawake Simba Queens.

-Kuna uwezekano mkubwa Pierre Lechantre akawa mkurugezi wa ufundi wa klabu hiyo au kuachana naye moja kwa moja mkataba wake ukiisha. Pia Mohamed Dewji ameanza kupanga safu yake ya Uongozi ndani ya klabu hiyo kuanzia mwezi ujao baadhi ya watendaji wa klabu ya Simba watapitishiwa panga ili kukidhi matakwa ya uwekezaji ndani ya klabu hiyo.

-Tangu Kocha Pierre Lechantre aanze kuifundisha klabu hiyo ameiongoza katika michezo 19 ikiwa 15 ya ligi kuu Tanzania Bara (vpl) na michezo 4 ya Kombe la Shirikisho Afrika (Caf Confederation Cup) katika michezo hiyo ameshinda mechi 13 ametoa sare mechi 5 na kufungwa mechi 1.

@yossima Sitta Jr.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.