Mashabiki Simba Kucheka Au Kununa Jumamosi Hii..


Timu ya Simba inashuka katika Uwanja wa Namfua mkoani Singida Jumamosi ikiwa ni siku ambayo inaweza kuwa ya furaha au huzuni kwa mashabiki wake.


Kikosi cha Simba endapo kitaibuka na ushindi Jumamosi basi kitakuwa kimekata kiu ya mashabiki wake kwa kutwaa taji la ubingwa msimu huu.


Iwapo Simba itapoteza au kutoa sare yoyote basi italazimika kusubiri hadi mechi inayofuata kwani inahitaji pointi mbili ili kujihakikishia ubingwa wao.


Hata hivyo, Ofisa wa Habari wa Simba, Haji Manara ameahidi kutoa ya moyoni endapo Simba itaibuka ana ushindi Jumamosi.
Manara ambaye amekuwa mtu wa tambo za kila aina kwa watani zake wa jadi Yanga anasubiria kwa hamu Simba kuukwaa ubingwa wa ligi ambao wameukosa kwa zaidi ya miaka takribani mitano.
Mpaka sasa Simba wana alama 65 huku Yanga wakiwa na pointi 48 pamoja na michezo mitatu mkononi.
Singida United wanawakaribisha Simba huku wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 4-0 kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza huku Wekundu wa Msimbazi wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja hadi sasa.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.