Abdi Banda Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Afrika Kusini.
Beki wa Tanzania, Abdi Banda ameshinda tuzo ya Mchezaji bora wa mwezi wa tano (may) wa klabu ya Baroka Fc ya Afrika Kusini.
Beki huyo aliisaidia Baroka Fc kutoa sare ya magoli 2-2 dhidi ya Bloemfontein Celtic huku yeye akifunga magoli yote mawili.
Banda na pacha wake Mote Kgoetyane mchezaji bora wa mwezi wa nne (april) wamepewa rand 5000 sawa na Tanzania Shilingi 907,375/- kwa kushinda tuzo hiyo.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.