Kamusoko Amtaja Mchezaji Huyu Wa Simba Kuwa Mchezaji Bora Kwa Msimu Huu.


Kiungo wa klabu ya Yanga, Thabani Kamusoko amemtaja mchezaji ambaye kwake amekuwa bora zaidi katika msimu huu waligi kuu Tanzania bara(2017/2018).

Kwa mujibu wa Kamusoko amemtaja straika machachali wa Simba sc, Shiza Kichuya kuwa ndiye mchezaji aliyefanya vizuri katika msimu wa huu.

Kichuya ambaye mpaka sasa ligi ikielekea ukingoni ameifungia Klabu yake magoli 7 na kuhusika katika pasi za mwisho kwenye magoli 20.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.