Taarifa Kutoka Simba Kuhusu Ushiriki Wao Kwenye Mashindano Ya Sportpesa Super Cup


Uongozi wa klabu ya Simba umethibitisha utapeleka full kikosi kenya kwenye michuano ya Sportpesa Super Cup itakayofanyika Kenya Kuanzia June 3-10 katika uwanja wa Karasani Nairobi Kenya.

Uongozi wa klabu hiyo umempa ratiba kocha wa kikosi hicho kikosi kuwa watavunja kambi baada ya kumalizika kwa michuano ya Kagame Cup itakayofanyika Tanzania Kuanzia katikati ya June hadi July Mwanzoni.

Akiongea kwa niaba ya Uongozi wa klabu hiyo mjumbe wa kamati Mtendaji wa klabu ya Simba Said Tully amesema

"Tutapeleka kikosi kamili ambacho kimecheza mechi za ligi kuu baada ya hapo tutarudi kupambana kwenye michuano ya kagame Cup ikiisha ndio tutavunja kambi"
Alisema Tully

Michuano ya Sportpesa Super Cup itakayoshirikisha timu 8 ikiwa 4 (Simba, Yanga, Singida, JKU) kutoka Tanzania na 4 (Gor Mahia, AFC Leopard, Kariobangi Sharks, Kakamega Homeboyz ) kutoka Kenya

Mshindi wa michuano hiyo atapata kombe na fedha dola 30,000 (69m) na pia atapata tiketi ya kwenda kucheza mchezo na Everton katika uwanja wa Goodison Park England.

Michuano hiyo itakuwa ya mtoani itaanzia hatua ya robo Fainali, nusu fainali na Fainali huku mshindi wa pili akipata kitita cha dola 10,000 (23m), Mshindi wa tatu atapata dola 7500 (17m), mshindi wa nne dola 5000 (11m) huku timu zote  zitapata dola 2500 (6m) kila moja kwa ajili ya maandalizi ya mchezo ila gharama za usafiri kwa timu za Tanzania kwenda Kenya itakuwa chini ya Sportpesa.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.