Bocco ashindwa kuvumilia Simba


Mshambuliaji wa Simba, John Bocco 'Adebayor' ameshindwa kuficha hisia zake kwa namna anavyofurahia kiwango chake alichokionyesha katika msimu huu wa ligi kuu ndani ya kikosi chake hicho cha Wekundu wa Msimbazi na amesisitiza , kwake ni historia itakayokumbukwa.


Bocco ambaye anashika nafasi ya pili kwenye ufungaji bora akiwa na mabao 14, amesema si jambo dogo kuonyesha uwezo ndani ya klabu kubwa na kongwe kama Simba na kutokana na hilo imemuongezea hali ya kujiamini zaidi.


"Nasikia faraja kuwa kati ya wachezaji muhimu waliofanikisha ubingwa wa Simba ambao ulikuwa unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa klabu hiyo, imenipa nguvu ya kujiamini na kuendelea kujituma zaidi,"anasema Bocco.


"Bahati nzuri zaidi, tunakabidhiwa kombe kwa heshima kubwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, John Pombe


Magufuli, kitu ambacho kitakuwa kumbukumbu katika maisha yangu yote ya soka."

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.