DEAL DONE: Azam Yakamilisha Kila Kitu Kwa Ngoma na Watampeleka Kutbiwa Afrika Kusini

Klabu ya Azam FC inatarajia kumpeleka Donald Ngoma katika Hospitali ya Vincent Pallotti jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya kumfanyia vipimo vya afya ili kuona ni kwa kiasi gani majeraha yaliyokuwa yakimsumbua yamepona.
Azam FC inaamini ya kuwa ujio wa nyota huyo kutoka nchini Zimbabwe aliyewahi kuchezea FC Platinum ya huko kabla ya kuhamia Yanga, ni sehemu tu ya mikakati ya benchi la ufundi na uongozi katika kuboresha kikosi kwenye eneo la ushambuliaji kuelekea msimu ujao.
Aidha kama mambo yataenda vizuri, uongozi wa Azam FC unaamini kuwa Ngoma atakuwa ni miongoni mwa nyota wapya wa timu hiyo watakaoonekana kwenye Kombe la Kagame (CECAFA Kagame Cup) linalotarajia kuanza hivi karibuni tukiwa kama mabingwa watetezi wa michuano hiyo
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.