Yanga Kurejea Kesho Kutokea Ethiopia.


Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea kesho Alhamisi, April 19 kutoka nchini Ethiopia ambako kimefanikiwa kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.

Yanga inatarajiwa kutua uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 7:10 usiku.

Muda wa kurudi umekuwa sio rafiki sana, pengine timu ingefika mapema zaidi ingepata mapokezi makubwa.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.