ASANTE SANA NADIR,KARIBU ABDALLAH SHAIBU


Beki Abdallah Shaibu 'Ninja' amedhihirisha sasa ameiva kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga hivyo kumpa nafasi ya kustaafu nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro'. Michezo miwili aliyocheza dhidi ya Wolaitta Dicha na mmoja dhidi ya Singida United imedhihirisha siku si nyingi Shaibu atakuwa beki wa kutegemewa katika kikosi cha Yanga.

Ukimuangalia kwa mbali unaweza ukadhani ni Nadir aliyerudi enzi za ujana wake! Wanafanana sana.

Bila shaka benchi la Ufundi litaendelea kumpa nafasi ili aweze kuimarika zaidi.

Huyu ndiye mrithi halisi wa Nadir ambaye huenda akastaafu kuitumikia Yanga mwishoni mwa msimu.

Nadir ndiye mchezaji aliyeitumikia Yanga kwa miaka mingi zaidi. Amecheza miaka 12!

Amevunja rekodi ya miaka 11 iliyokuwa ikishikiliwa na Fred Mbuna.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.