YANGA: Hili likitokea basi ubingwa wa Simba


Yanga kwa sasa inaendelea kuwa chini ya kocha msaidizi, Shadrack Nsajigwa baad aya aliyekuwa kocha mkuu George Lwandamina kuondoka klabuni hapo, lakini upande wa pili ni kuwa timu hiyo ina wkati mgumu kwenye mchakato wa kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom. 

Yanga inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo lakini ina wakati mgumu kwa kuwa imezidiwa pointi nane na wapinzani wao wa jadi, Simba huku zikiwa zimesalia mechi chache kabla ya ligi kumalizika. 

Lakini pamoja na hivyo, Yanga limesema kuwa, kwa sasa haijakata tamaa ya ubingwa, labda itokee zimesalia mechi mbili ndiyo wataona hawana chao. Yanga ambayo Jumatano iliyopita ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Singida United katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kusafiri kwenda Ethiopia, Jumapili ya wikiendi hii kwa ajili ya mchezo wa wa Kombe la Shirikisho. 

Kocha Msaidizi wa Yanga, Nsajigwa ambaye ni beki na nahodha wa zamani wa timu hiyo amesema bado hawajatoka kwenye mbio za ubingwa ingawa matokeo ya sare dhidi ya Singida si mazuri kweo. 

Akifafanua zaidi Nsajigwa alisema: “Mechi zimebaki nyingi ambazo ni kama nane hivi jambo ambalo huwezi kututoa kwenye mbio za ubingwa labda ingekuwa zimebaki mechi mbili sawa tungesema hivyo lakini siyo sasa ambapo lolote linaweza kutokea.”

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.