MKWASA AHUSISHWA KUACHIA NGAZI, YANGA WATOA KAULI HII


Baada ya uongozi wa Yanga jana kuahirisha Mkutano na Waandishi wa Habari katika makao makuu ya klabu hiyo, imeelezwa kuwa Katibu Mkuu, Charles Boniface Mkwaswa, alipanga kujiuzulu.

Yanga ilitangaza juzi kuwa itaitisha mkutano na wanahabari jana majira ya saa saba mchana lakini ulishindwa kufanyika kutokana na sababu zisizozuilika.

Kwa taarifa za chini ya kapeti zinaelezwa Mkwasa alipanga kuachia ngazi lakini Yanga wamekanusha taarifa hizo kwa kushindwa kutoa jibu rasmi kuhusiana na sual hilo.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa klabu, Dismas Ten, alisema kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo hivi sasa kutokana na kubanwa na maandalizi ya safari kuelekea Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Wolaitta Dicha FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Kupitia Radio One, Ten alisema kuwa si muda mwafaka kuongelea jambo hilo kama litakuwepo litaelezwa rasmi lakini kwa sasa fikra zote zinahamishiwa kwenye mchezo wa kimataifa.

Yanga inatarajia kuondoka muda wowote kuelekea Ethiopia kucheza na Wolaitta Dicha FC katika mchezo wa mkondo wa pili ambapo mechi ya kwanza iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.