Kocha Wa Viungo Wa Yanga Kubeba Mikoba Ya Lwandamina.

       ==>>Aliyekaa Upande Wa Kushoto Wa Lwandamina.
Wakati Yanga ikiwa kwenye mchakato wa kumpata kocha wa kuchukua nafasi ya George Lwandamina, kocha msaidizi Noel Mwandila ndiye anayekuwa kocha Mkuu kwa sasa akisaidiana na Shedrack Nsajigwa, imefahamika.

Baada ya Kamati ya Utendaji kukutana juzi, wajumbe walikubaliana kuwa makocha hao waendelee na majukumu yao ya sasa hadi pale itakapotangazwa vinginevyo.

Mwandila aliletwa na kocha George Lwandamina kuwa msaidizi wake. Lakini yeye ameendelea na majukumu yake katika klabu ya Yanga hata baada ya kuondoka kwa bosi wake huyo.

Hata hivyo huenda nae akajiunga na ZESCO mwishoni mwa msimu hivyo Yanga inalazimika kusaka kocha mwingine.

Baadhi ya majina ya makocha wanaotajwa tajwa ni pamoja na Ettiene Ndairagije; kocha wa Mbao FC, Nsanzurwino Ramadhani anayeinoa klabu ya Mbeya City.

Hans van Pluijm alikuwemo katika orodha ya makocha waliokuwa wanawaniwa lakini hilo halitawezekana kwani huenda kocha huyo akajiunga na Azam FC mwishoni mwa msimu baada ya klabu hiyo kutangaza kutomuongeza mkataba kocha wake.

Inadaiwa kuwa Pluijm tayari ameshasaini mkataba wa awali katika klabu ya Azam FC.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.