TFF kuipiga 'tafu' Yanga Kimataifa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa Katibu Mkuu wake Wilfred Kidao, limeweka wazi kuwa linajipanga kuhakikisha linaipiga 'tafu' Yanga katika mchezo wake wa marudiano katika Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wahabeshi Wolayta Dicha utakaopigwa tarehe 18 mwezi huu, huko Ethiopia.
Lengo kubwa la TFF kufanya hivyo ni kutaka kuiona Yanga inasonga mbele hatua ya makundi ya michuano hiyo kwani ndiyo wawakilishi pekee waliobakia kimataifa msimu huu.
“Tutaipatia muda wa kutosha wa maandalizi lakini pia tutatuma wawakilishi wetu Ethiopia kabla ya mechi hiyo kwa ajili ya kwenda kuweka mambo sawa ili siku itakapoenda huko isikumbane na usumbufu.
“Michuano hii ni ya kimataifa na ikifanya vizuri sifa itakuwa siyo kwa klabu pekee bali kwa taifa zima la Tanzania, kwa hiyo inatubidi tushirikiane nao kwa karibu kabisa ili kuhakikisha inapata matokeo mazuri katika mchezo wake huo wa marudiano,” alisema Kidao.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.