Tetesi za Usajili Ulaya Leo Jumatano Aprili,25 2018


Arsenal inaamini inaweza kumshawishi aliyekuwa mkufunzi wa Barcelona Luis Enrique kuchukua mahala pake Arsene Wenger kama meneja wake.

Mkuu wa uhusiano katika klabu hiyo hiyo Rail Sanllehi alifanya kazi na Enrique katika klabu ya Barcelona.. (Mirror)

Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Carlo Ancelotti, ambaye ni mkufunzi mwengine anayepigiwa upatu kumrithi Wenger amepewa kazi ya kuifunza timu ya taifa ya Italy.(Times - subscription required)

Mwenyekiti wa zamani wa Arsenal Peter Hill-Wood, ambaye amemuajiri Wenger mwaka 1996, amesema kuwa ni wakati kwamba mkufunzi huyo anafaa kuondoka. (Star)

Manchester City haina mpango wa kumuuza beki John Stones, 23, na raia huyo wa Uingereza yuko katika mipango ya mkufunzi Pep Guardiola.

Guardiola anataka kushirikiana tena na kiungo wa kati wa Barcelona Andres Iniesta katika klabu ya Manchester City.

Mchezaji huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 33 pia amehusishwa na klabu ya ligi ya kwanza nchini Ufaransa PSG mbali na kuelekea China.

Manchester United italazimika kutoa kitita cha £40m pamoja na beki wa Uingereza mwenye umri wa miaka 22 ili kuweza kumununua beki mwenza wa Uingereza na Tottenham Danny Rose, 27, kutoka Tottenham.(Sun)

Mbali na Rose, mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anataka kumsaini beki wa kulia mwisho wa msimu huu. (Guardian)

Real Madrid italenga kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski, 29, mwisho wa msimu huu kama suluhu ya muda mfupi huku wakiendelea kusaka saini ya mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 24. (Sun)

Leicester inapanga kumsajili beki wa kulia wa Porto Ricardo Pereira, 24. Mchezaji huyo wa Ureno ana kipengee cha £36m kwa yeye kuondoka katika klabu hiyo (Mirror)

Beki wa zamani wa Chelsea na Uingereza John Terry, 37, anaweza kuongeza kandarasi yake na klabu hiyo hadi mwisho wa msimu huu (Talksport)

Washindi wa ligi ya mabingwa nchini Uingereza Wolves wanataka kumsajili beki wa Manchester City Eliaquim Mangala, 27, na hawatakuwa na tatizo lolote kumlipa raia huyo wa Ufaransa mshahara wa £85,000 kwa wiki. (Sun)

Tottenham imeanza mazungumzo na beki wa timu ya vijana nchini Uingereza Kyle Walker-Peters, 21. (ESPN)

West Ham itampatia beki wa Ireland Declan Rice, 19, mkataba wa muda mrefu . (Evening Standard)

Chelsea haitamuuza mshambuliaji wake wa Uhispania Alvaro Morata, 25, ama kiungo wa kati wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 23, hadi pale watakapotaka kuondoka Stamford Bridge.. (Telegraph)

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.