TANZIA: Haruna Niyonzima Apata Msiba



Kiungo wa Simba Haruna Niyonzima amepata msiba wa kufiwa na dada yake, msiba uliotokea leo nchini Rwanda.

Niyonzima tayari yuko jijini Dar es salaam akishughulikia usafiri wa kuelekea nchini Rwanda kuhudhuria msiba huo.

"Nimepata matatizo bwana, nimefiwa na dada yangu nyumbani Rwanda na hivi sasa niko hapa nyumbani nikijiandaa kwa ajili ya safari. Kwa sababu ni jambo la kushtukiza ndiyo nahangaikia ndege kuona kama naweza kuondoka,"amesema Niyonzima muda mfupi baada ya kuwasili jijini Dar es salaam akitokea Morogoro.

Niyonzima huenda akaukosa mchezo dhidi ya Yanga utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Jumapili April 29 2018

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.