Tayari TFF Imeweka Hadharani Viingilio Vya Mchezo Kati Ya Mbeya City Dhidi Ya Yanga.
Klavu ya Yanga inatarajiwa kushuka dimbani kesho kuwakabili mbeya City kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara unaotarajiwa kupiwa katika uwanja wa Soko nne mjini humo.
Katika mchezo huo namba 178 utakaofanyika saa 10 jioni Kiingilio cha chini kitakuwa shilingi Elfu Saba(7,000) wakati kiingilio cha juu kitakuwa shilingi Elfu Thelathini.
Jukwaa la VIP A itakuwa shilingi Elfu Thelathini (30,000),VIP B na C shilingi Elfu Ishirini (20,000) na Upande wa Mzunguko kwenye viti vya rangi ya Chungwa,Bluu na Kijani itakuwa shilingi Elfu Saba (7,000)
Tiketi tayari zimeanza kupatikana kupitia Selcom
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.