Simba Kushuka Dimbani Leo Bila Nyota Huyu.
Kikosi cha Simba kinashuka dimbani Uwanja wa Samora mjini Iringa kikiwa mgeni dhidi ya Lipuli.
Simba itakuwa inacheza bila kiungo wake Jonas Mkude ambaye atakosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
Mkude atalazimika kusubiri mechi dhidi ya watani zake wa jadi utakaopigwa Aprili 29 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kiungo James Kotei ndiye atakuwa mbadala wa Mkude katika sehemu ya kiungo kutokana na kufanana aina ya mchezo wanaocheza.
Mechi dhidi ya Lipuli leo itaanza saa 10 kamili jioni.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.