Mtibwa Waitahadharisha Simba sc..
Afisa Habari wa klabu ya soka ya Mtibwa Sugar Thobias Kifaru Ligalambwike, amewaomba mashabiki wa timu ya soka ya Simba kuwa na utulivu pale watakapoyapokea matokeo ambayo hawakuyatarajia.
Kifaru amesema anajua matokeo mazuri waliyoyapata katika michezo miwili iliyopita kwa kuwatoa Azam kwenye michuano ya FA na kuwafunga Singida United mabao 3-0 yamewapa nguvu zaidi kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba Jumatatu hii.
"Hatutakubali kamwe kuwa njia rahisi kwa Simba kutwaa ubingwa, kwa kasi ambayo tunayo sasa tunakila sababu ya kujivunia kikosi kilichobora, wale wanaojiita mashabiki wa Simba wawe watulivu wasubiri hadi dakika 90 watakachokipata basi wakipokee," Kifaru amesema.
Jambo muhimu
Mtibwa Sugar ambao wameshinda mchezo mmoja kati ya michezo sita ya mzunguko wa pili watajitupa uwanjani April 9, 2018 kucheza na Kinara Simba SC ambao hawajapoteza mchezo wowote mpaka sasa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Katika mzunguko wa kwanza timu hizo zilipokutana katika uwanja Uhuru jijini Dar es Salaam walitoka sare ya bao 1-1, Mtibwa ndio waliokuwa wa kwanza kupitia kwa Stamil Mbonde kabla ya Emmanuel Okwi kusawazisha katika dakika za mwisho kabisa.
Mechi za raundi ya 23 Jumapili April 8, 2018
Mbeya City Vs Azam FC - Sokoine, Mbeya.
Stand United vs Njombe Mji - CCM Kambarage, Shinyanga.
Ruvu Shooting vs Tanzania Prisons - Mabatini, Pwani.
Ndanda FC vs Kagera Sugar - Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.