Mchezo Kati Ya Yanga Na USM Alger Kombe La Shirikisho Kupigwa Usiku, Hii Hapa Tarehe na Muda Kamili Utakapochezwa Mchezo Huo.
Mchezo wa kwanza wa kundi D kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya USM Alger utapigwa nchini Algeria Jumapili ya May 06 saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Hiyo itakuwa ni wiki moja baada ya mpambano wa watani wa jadi dhidi ya Simba utakaopigwa Jumapili ijayo April 29 kwenye uwanja wa Taifa.
Kuelekea mchezo huo muhimu, kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema maandalizi wanayofanya sasa mkoani Morogoro sio kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba pekee.
Bali ni maandalizi ya pamoja na michuano ya kombe la Shirikisho ambayo imepewa kipaumbele zaidi kutokana na 'ukwasi' wake
Yanga imepangwa kundi D pamoja na USM Alger, Rayon Sports na Gor Mahia. Kundi ambalo kama Yanga itazichanga vyema karata zake inaweza kutinga robo fainali.
Licha ya kuwa imewahi kutwaa taji la ligi ya mabingwa Afrika, USM Alger kwa sasa sio moja ya timu za kuogofya katika ligi ya Algeria na soka la Afrika kwa ujumla.
Katika msimamo wa ligi ya Algeria, USM inashika nafasi ya sita ikiwa imejikusanyia alama 39 kutoka michezo 27 ikiachwa kwa alama 11 na vinara wa ligi hiyo CS Constantine.
Yanga inaweza kupata matokeo nchini Algeria.
Bila shaka viongozi watawahi kwenda nchini humo mapema kuweka mambo sawa kabla ya kikosi cha Yanga kufika.
Algeria, Misri na Tunisia zinasifika kwa figisu za nje ya uwanja.
Yanga itacheza mchezo wake wa pili kwenye uwanja wa Taifa dhidi ya Rayon Sports May 16.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.