Kocha Lechantre Kuachana Na Simba, Hii Hapa Timu Atakayoinoa Akiondoka

Kocha mkuu wa Klabu ya Simba  Mfaransa Pierre Lechantre anaweza akaondoka klabuni humo na hii ni baada ya kuomba kazi ya kufundisha timu ya taifa ya Cameroon.

Jina lake ni miongoni mwa majina  yaliyotajwa kwenye Orodha ya makocha walioomba kazi ya kuifundisha Cameroon.

Kwa sasa anasubiri mchujo ambao utabakisha majina matatu yatakayofanyiwa usaili na mmoja wao kupewa kazi ya kuwa kocha mkuu wa nchi hiyo.

@yossima Sitta Jr.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.