Madrid Yainyuka Bayern Munich UEFA, Mguu Mmoja Fainali.

Real Madrid imeendeleza umwamba katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Bayern Munich mabao 2-1 kwenye uwanja wa Allianz Arena.

Real ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo akitwaa mara mbili mfululizo na kuna uwezekano mkubwa wa kuingia fainali.

Joshua Kimmich aliifungia Bayern bao la kwanza dakika ya 28 kwa shuti baada ya kupokea pasi ya James Rodriguez.

Marcelo aliisawazishia Real bao hilo dakika ya 44 kwa shuti la chini chini akimalizia mpira wa Danny Carvajal.

Mshambuliji Marco Asensio aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Isco aliifungia Real bao la pili dakika ya 57 baada ya kupokea pasi safi ya Lucas Varquez.

Mchezo wa marudiano utakaofanyika Santiago Bernebeu Jumanne ijayo na mshindi wa jumla ataingia fainali.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.