Mbonde Asema Haya Kuelekea Mechi Ya Simba Na Yanga.


Beki wa klabu ya Simba, Salum Mbonde, amesema kuwa wanaendelea na maandalizi ya mchezo dhidi ya Yanga utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa Jumapili ijayo, April 29 2018.

Mbonde ambaye amerejea kikosini hivi karibuni baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeruhi, amesema mechi hiyo itakuwa si nyepesi wala ngumu, kwani atakayejipanga atapata matokeo.

Mbonde ameeleza kuwa mechi inayokutanisha timu hizo za Kariakoo inakuwa ni ya aina yake na si rahisi kutabirika kama wengi wanavyodhani.

Akizungumza kupitia kipindi cha Spoti leo cha Radio One, Mbonde amesema ana shauku kubwa ya kucheza mechi hiyo itakayopigwa Aprili 29 2018.

Simba na Yanga ziko mkoani Morogoro zikiendelea na maandalizi ya mchezo huo

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.