Kocha Pya Yanga Aja Na Mfumo Tofauti..


Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameonyesha sio mtu wa masihara ambapo kwenye siku yake ya kwanza tu mkoani Morogoro amedhihirisha uwezo wake.

Zahera alitua mkoani Morogoro jana kwa lengo la kuonana na wachezaji pamoja na benchi la ufundi. 

Baada ya kufanya kikao kifupi, Zahera alielekea moja kwa moja uwanja wa Highlands ambao Yanga inatumia kwa mazoezi yake.

Mara moja akaanza kutoa maelekezo kwa wasaidizi wake sambamba na wachezaji.

Zahera anayependelea zaidi mpira wa 'ki-Brazil', aliwaongoza wachezaji kufanya mazoezi ya kumiliki mpira akiwataka wahakikishe hawapotezi, sambamba na kupiga pasi za haraka kuelekea langoni kwa mpinzani. 

Leo Yanga inaendelea kujifua kwenye uwanja wa Highlands kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa Jumapili ijayo, April 29 2018.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.