Alichosema Niyonzima Kuelekea Mchezo Wa Simba Na Yanga..


Kiungo mahiri wa timu ya Simba, Haruna Niyonzima ameeleza kuwa kama wataibuka na ushindi kwenye mchezo dhidi ya watani wao Yanga Jumapili ijayo watakuwa wamekaribia kabisa kutwaa ubingwa msimu huu.

Niyonzima hatakuwa sehemu ya mchezo huo kutokana na kupata msiba wa dada yake ambapo alisafiri jana usiku kuelekea nchini Rwanda kufuatilia suala hilo.

Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga alisema kama watapata pointi tatu kwenye mchezo huo watakuwa juu kwa tofauti ya pointi 14 hivyo watakuwa wameukaribia ubingwa.

Licha ya kutokuwepo kwenye mchezo huo Niyonzima alisema wachezaji wengine watakaopata nafasi kushuka dimbani anaamini watapeperusha vizuri bendera ya Simba na ushindi utapatikana.

"Ni mechi muhimu kwetu, kama tutapata ushindi tutakuwa kwenye mazingira mazuri ya kuchukua ubingwa msimu huu.

"Mimi sidhani kama nitakuwepo katika mchezo huo nimepata msiba wa dada yangu lakini naamini yoyote atakaye pewa nafasi atafanya vizuri na tutashinda mchezo," alisema Niyonzima.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.