Kipa Wolaitta Dicha Aapa Kuiondoa Yanga Mcjezo Wa Marudiano.


Mlinda Mlango wa timu ya soka ya Welayta Dicha Besufikad Teferi Mola amesema hawajakata tamaa ya kutinga hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika licha ya kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Dar Young Africans katika mchezo wa duru ya kwanza uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mola amesema wameshindwa kucheza vizuri na kuruhusu mabao hayo kutokana na kutowafahamu kabisa Yanga, lakini kwa kuwa wameshawasoma na kutambua udhaifu wao basi watautumia watakapokutana katika mchezo wa marudiano baadae mjini Awassa.

"Tumefungwa kwa sababu kwanza tulikuwa hatuwafahamu vizuri wapinzani wetu, tulikuwa tunawasikia tu wanavyocheza lakini sasa tumewajua, tumejua tucheze vipi ili kuweza kuwafunga, tunaenda kwetu si ndio, tutahitaji kufunga mabao mengi! sasa tutashinda na tutasonga mbele amini nikuambiavyo," Mola amesema mara baada ya mchezo huo kumalizika.

Ushindi mzuri kwetu

Aidha kwa upande wa nahodha wa Yanga Nadir Haroub amesema ilikuwa ni lazima wapate matokeo ya ushindi na hilo linawapa moyo wa kusonga mbele katika hatua ya makundi.

"Tulikuwa tunahitaji sana ushindi huu, mabao mawili si haba ni mtaji tosha, lakini hatutabweteka, lazima tukaze hata tunapokuwa ugenini, kwanza tusiruhusu bao lakini pia tutafute bao, siwezi kusema tayari tumeshaingia hatua ya makundi lakini naiona nafasi," Haroub amesema.

Mchezo wa marudiano utafanyika nchini Ethiopia katika uwanja wa Hawassa na Welayta Dicha watahitaji kushinda kwa zaidi ya mabao matatu ili kufuzu kwa mara ya kwanza katika hatua ya makundi, aidha Yanga wao watahitaji sare yoyote ama ushindi kuingia hatua ya makundi kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.